HII NI BLOG YA KIMICHEZO NA INA HUSISHA MAISHA YA MASTER WA BONGO NA DUNIA KIUJUMLA
Monday, September 8, 2014
Kiongozi wa upande wa upinzani wa Msumbiji, Renamo, Alfonso Dhlakama amesaini mkataba wa amani na rais Armando Guebuza katika mji mkuu wa Maputo, na kumaliza mvutano uliodumu kwa miaka miwili. Bwana Dhlakama, ambaye amejitokeza kutoka mafichoni, amesema atagombea katika uchaguzi wa urais mwezi ujao. Mzozo huo ulitishia ukuaji wa uchumi katika taifa hilo. Rais Guebuza anaachia ngazi Oktoba 15 baada ya kumaliza mihula miwili. Waziri wa ulinzi anatarajiwa kugombea urais kupitia chama tawala cha Frelimo
No comments:
Post a Comment