ANDY BEATZ
HII NI BLOG YA KIMICHEZO NA INA HUSISHA MAISHA YA MASTER WA BONGO NA DUNIA KIUJUMLA
Monday, September 8, 2014
"GETO" LA BALOTELLI? Mario Balotelli ndio kwanza amerejea England, kwa mara ya pili, lakini inaonekana haijamchukua muda mrefu kugonga vichwa vya habari, safari hii kwa kuonesha "ladha" ya mitindo na mambo anayopenda. Mchezaji huyo wa Liverpool aliyenunuliwa kutoka AC Milan kwa pauni milioni 16, amekuwa akitafuta nyumba, na inasemekana ameichagua hii (katika picha) iliyopo nje ya mji, - eneo la Helsby, Cheshire - na kufanya ndio "keja". Na kama picha hizi pamoja na habari ambazo zimeandikwa na magazeti na tovuti kadhaa hapa Uingereza ni za kuaminika, basi inaonekana Balotelli ameonesha 'staili' yake kwa 'kuteua' jumba hili ambalo thamani yake ni pauni milioni 4.7. Nyumba hii ina vyumba vitano, ikiwa pamoja na kila kitu ambacho mchezaji soka , Kijana, milionea anahitaji. Vitu 'muhimu' kama bwawa la kuogelea, sauna, chumba cha kuhifadhia mvinvyo (wine cellar), sehemu ya kutua helikopta, uwanja wa mpira.. Na vingine 'vidogovidogo
Kiongozi wa upande wa upinzani wa Msumbiji, Renamo, Alfonso Dhlakama amesaini mkataba wa amani na rais Armando Guebuza katika mji mkuu wa Maputo, na kumaliza mvutano uliodumu kwa miaka miwili. Bwana Dhlakama, ambaye amejitokeza kutoka mafichoni, amesema atagombea katika uchaguzi wa urais mwezi ujao. Mzozo huo ulitishia ukuaji wa uchumi katika taifa hilo. Rais Guebuza anaachia ngazi Oktoba 15 baada ya kumaliza mihula miwili. Waziri wa ulinzi anatarajiwa kugombea urais kupitia chama tawala cha Frelimo
BREAKING NYUZI: HABARI ZA HIVI PUNDE!! AJALI NYINGINE MBAYA MAENEO YA KIEGEYA GAIRO, GARI LA ABIRIA KUTOKA DAR-TABORA LIMEPATA AJALI MBAYA KIASI KWAMBA WATU KARIBIA 48 WAMEPOTEZA MAISHA. NI DK 6 ZILIZOPITA..PICHA HAZIFAI KUONWA NA MIMI NIKO ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA UOKOZI..VIONGOZI MBALI MBALI WA SERIKALI TUNAO HAPA..KWAKWELI NI MAJONZI VILIO NK. Air BUS DAR-TABORA.
Newer Posts
Older Posts
Home
Subscribe to:
Posts (Atom)